Masomo ya biblia



 Ev. John Mafuru
0764736335



SOMO: JE, MTU AKIFA ANAENDA WAPI?
KIFO ni mgeni asiyezoeleka miongoni mwa binadamu wengi. Kila mtu anapofiwa na ndugu, mke,mume jamaa na rafiki wa karibu huumia sana na wengine mpaka hukata tamaa ya kuendelea kuishi na wengine huamua kujiua. Kifo huleta machungu sana katika maisha ya mwanadamu na ni tokeo la dhambi iliyofanywa na wazazi wetu wa kwanza. Imani nyingi zimeibuka zikizungumzia kifo kwa namna mbalimbali, Imani nyingine zinaamini mtu akifa akiwa ametenda mambo mema moja kwa moja anakwenda mbinguni, akifa amefanya matendo mabaya moja kwa moja anaenda motoni, Imani zingine zinafundisha kuwa mtu akifa kama anadhambi ataombewa na viongozi wa dini naye atasamehewa na kuingia mbinguni, zingine zinafundisha mtu akifa kama katenda mema atazaliwa sehemu katika familia ya kitajiri au kifalme na kama katenda mabaya atazaliwa katika familia duni au kiumbe kingine kama mjusi n.k. Imani zingine zinafundisha mtu akifa anakuwa hai na ndugu au jamaa au watoto wanaweza kuwasiliana nae wanapohitaji. Kwa ufupi kuna Imani nyingi sana kuhusu mtu anapokufa anakwenda wapi.
Mpenmzi msomaji usiogope kusikia hayo, sasa tukiulize kitabu kitakatifu (Biblia) je mtu akifa hatima yake ni nini na anakuwa wapi. KIFO katika kamusi ya Oxford imetafsiriwa kama “End of something” mwisho  wa kitu fulani. Ili kupata ufafanuzi mzuri kwanza tujue nini kinamfanya mtu kuwa HAI. Uhai ni Mwili jumlisha pumzi “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai”. Mwanzo 2:7. Tazama hii UHAI=Mavumbi+Pumzi. KIFO=Mavumbi-Pumzi ya Uhai.
Katika Mwanzo 2:7 tunapata maneno mawili nalo ni MWILI  ambao ulitokana na mavumbi au ardhi na PUMZI YA UHAI ambayo Mungu aliipulizia puani kwa mwanadamu akawa kiumbe hai. Baada ya dhambi Mungu alisema maneno haya, Mwanzo 3:19 “kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa, kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi” akiwa na maana kwamba kwa kuwa MWILI ni mavumbi basi anapokufa mtu mwili unarudi mavumbini ndio maana mtu yoyote akifa lazima anazikwa chini ya ardhi na anaoza hukona kuwa udongo. Ayubu 27:3 inasema hivi “kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu, na roho ya Mungu I katika pua yangu” inamaana kuwa roho ni sawa na Pumzi ambayo Mungu aliipulizia puani mwa mwanadamu akawa hai.
Kwa mwandamu kifo kina maana ni utengano kati ya MWILI na PUMZI YA UHAI. Kunapokuwa na utengano huu hapo ndo mwisho wa mwanadamu na katika ulimwengu huu kifo siku zote ni kipya hakizoeleki kabisa. Hebu fuatana name katika mafungu haya ili kujifunza Zaidi.




Muhubiri 12:7 “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa”. Hivyo mtu anapokufa haendi popote bali mwili hurudi mavumbini na Mungu anaichukua Pumzi yake ya uhai. Pia Muhubiri 9:5 inasema “kwaq sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa,lakini wafuhawajui neon lolote,wala hawana ijara tena,maana kumbukumbu lao limesahauliwa”. Mtu anapokufa habari zake zinaishia hapo hajui lolote wala hawezi fanya lolote hivyo wale wenye Imani ya kwamba mtu akifa mnaweza kuongea nae Mungu wa mbinguni ameshakuelimisha ya kwamba mtu akifa basi habari zatoweka. Soma pia Zaburi 115:17. Yesu kristo katika Yohana 11:11 na kuendelea alifananisha kifo na usingizi (kisa cha lazaro), chukulia mfano ya kwamba ukilala je unakumbuka lolote au unajua kinachoendelea duniani.




Tumekwisha elewa kwamba mtu anapokufa mwili unarudi mavumbini na roho au pumzi ya uhai uichukua Mungu aliyeipulizia. Je nini kitafuata baada ya mtu kufa?. Kwasisi tulio hai tumaini tunalo ambalo Mungu amelifununa kwetu kupitia manabii wake na mwanawe mpendwa Yesu kristo. Yohana 5:28-29 inasema hivi Msistaajabie maneno hayo,kwa maana saa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu, na hili jambo litatokea pale yesu kristo atakapo kuwa anarudi mara ya pili hapa duniani ndipo wafu wote watasikia parapanda ikilia waliokufa katika yesu watafufuliwa kwanza na kuvikwa kutokufa soma pia 1Thesalonike 4:15, 16 na 1Korintho 15:51-54.
Ewe mpenzi msomaji usiwe na wasiwasi juu ya kifo kwa maan atumaini lipo katika kristo yesu, Ufunuo 1:17-18 inasema “Nami nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa.Akaweka mkonowake wa kuumejuu yangu, akasema, usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho na aliye hai;name nalikuwa nimekufa na tazama ni hai hata milele.Nami ninazofunguo za mauti na za kuzimu.” Usomapo ujumbe huu njoo sasa kwa Yesu ,mshindi na aliye na fungua za mauti ili uweze kuwa hai hata ukifa kwaa maana Yesu ndiye njia na uzima.

Barikiwa mpenzi msomaji na usisite kuwasiliana nasi kwa jambo lolote liwe swali au ufafanuzi wa mada Fulani au maoni na ushauri.


Comments